Sheikh Bir Ali Mumin, Naibu Mufti Mkuu wa Bulgaria akijibu makala iliyojaa uongo ya Profesa Vasilef wa kitivo cha filosofia katika Chuo Kikuu cha Sofia cha Bulgaria iliyochapiswa katika gazeti la nchini humo la Duma chini ya kichwa cha 'Upana wa Umajumui wa Kiislamu', amesema kuwa: "Vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na radio na televisheni zina nafasi kubwa katika kuiarifisha dinia ya Kiislamu'.
Katika mahojiano na gazeti la Sega la Bulgaria Sheikh Mumin alipoulizwa, 'kwa nini Waislamu wanazingatiwa sana wakati wa uchaguzi wa bunge na suala la Uislamu wa kufurutu mipaka kuongezeka katika duru za kijamii?. Alijibu kwa kusema: 'Ninafikiri chanzo chake si uchaguzi tu. Kuna tatizo katika kukubali fikra na itikadi za wengine. Kuna haja ya kujuana zaidi'.
Amesema baadhi ya vyombo vya habari vinajadili masuala makubwa bila kuwa na ufahamu sahihi wa dini na hili hupelekea kuakisiwa visivyo ukweli wa filosofia ya dini'. Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona Uislamu unaarifishwa kama tishio. Naibu Mufti wa Bulgaria amesema fikra hii potofu hasa ilipata nguvu baada ya matukio ya Septemba 11.
Kuhusu baadhi ya watu ambao wanafurutu mipaka kwa jina la Uislamu na kutekeleza vitendo vya utumiaji nguvu, Sheikh Mumin amesema: "Katika suala hili mafunzo ya dini hayana kosa lolote. Walio na dosari ni wanaadamu wanaofasiri visivyo mafunzo ya kidini na kutoa maoni yao ambayo husababisha matatizo'. 401681