IQNA

Kamati ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kutembelea Gaza

9:43 - May 10, 2009
Habari ID: 1776057
Kamati ya wataalamu wa uchunguzi ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa ilitoa taarifa ikisema kuwa hivi karibuni itaanzisha shughuli zake za uchunguzi huko katika Ukanda wa Gaza kwa lengo la kujua ukweli kuhusiana na hujuma ya kijeshi iliyofanywa huko na utawala ghasibu wa Israel.
Kwa mujibu wa gazeti la Khaleej Times, kwa mara nyingine tena kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa imeutaka utawala wa Israel kushirikiana nayo kuhusiana na suala hilo. Mwezi uliopita utawala wa Tel Aviv ulitangaza kwamba hautashirikiana kwa nia yoyote ile na kamati hiyo. Richard Goldstone, Mwendesha Mashtaka wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na ambaye ndiye mkuu wa hivi sasa wa kamati hiyo ya wataalamu wanne, ambayo ilibuniwa mwezi uliopita kwa ajili ya kufuatilia jinai za utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, amesema kuwa uchunguzi wa kisheria na usiopendelea upande wowote ule kuhusiana na suala hilo utakuwa ni kwa mslahi ya wote, na pia kwa faida ya kuimarishwa amani na usalama katika Mashariki ya Kati. Katika upande wa pili, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kwamba utawala wa Israel ulitekeleza jinai za kivita dhidi ya Wapalestina kwa kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa za fosforasi nyeupe dhidi yao. 402032
captcha