IQNA

Duru za mafunzo ya Qur'ani nchini Saudia

9:42 - May 10, 2009
Habari ID: 1776058
Duru ya 75 ya mashindano ya kitaifa ya masomo ya Qur'ani Takatifu, imeanza siku ya Jumamosi nchini Saudi Arabia. Duru hiyo ya masomo inadhaminiwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya na Kuhifadhi Qur'ani katika mkoa wa Taif.
Masomo hayo yamepangwa kuchukua muda wa wiki sita. Lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kufanya usomaji wa Qur'ani kuwa suala la kuzingatiwa na umma kwa ajili ya wananchi wa Sauadi Arabia. Mashindano hayo yanaandaliwa bure na bila ya usajili wowote wa majina. Mashindano hayo yatafanyika katika hatua tatu za mwanzo, wastani na ya juu. 401988
captcha