Hayo yamesemwa na Amin Puya ambaye ameongeza kuwa tunapasa kujifunza usomaji sahihi wa Qur'ani kwa kusoma misingi na kanuni sahihi za usomaji kitabu hicho. Akizungumza hivi karibuni mbele ya wapenzi wa Qur'ani mjini Tehran, Puya amesema kuwa usikilizaji wa visomo vya Qur'ani vya wasomaji mashuhuri wa kitabu hicho cha wahyi, na hasa cha Mahmoud Khalil al-Huswari, humsaidia sana msomaji kusoma kwa njia sahihi kitabu hicho. Amesema, kisimo cha tartil na tajweed cha msomaji huyo husaidia sana katika kumwezesha msomaji kusoma vyema aya za Qur'ani Tukufu. 402103