IQNA

Mfuko mpya wa uwekezaji wa Kiislamu kuzinduliwa Malaysia

23:32 - May 10, 2009
Habari ID: 1776596
Mfuko mpya wa uwekezaji wa Kiislamu nchini Malaysia unaodhaminiwa na Shirika la Uwekezaji la Kuwait utazinduliwa .
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA wa kusini-mashariki mwa Asia, mfuko huo wenye thamani ya dola milioni 150 unatazamiwa kuzinduliwa katika mustakabali usio mbali na utatekeleza shughuli zake kwa msingi wa sheria za Kiislamu katika uga wa uchukuzi baharini.
Mfuko huu unoanzishwa kwa ushirikiano wa shirika la bima la Uingereza la FSF utatoa huduma kwa muda wa miaka saba na baada ya hapo kandarasi yake inaweza kutiwa saini upya kila mwaka baada ya hapo.
Katika miaka ya hivi karibuni uwekezaji wa Kiislamu na utekelezaji shughuli za kiuchumi kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu umeongezeka sana nchini Malaysia . Hiyo maajuzi Zitti Akthari Aziz rais wa Benki Kuu ya Malaysia alitangaza kuunga mkono kikamilifu uwekezaji wa Kiislamu nchini humo.
Amesema kuwa, kwa mujibu wa mapendekezo ya marekebisho ya sheria yaliyowasilishwa katika bunge la Malaysia, mahakama za nchi hiyo zitalazimika kutumia wataalamu wa Kiislamu katika masuala yanayohusiana na uwekezaji wa Kiislamu. 402063
captcha