IQNA

Kikao cha kimataifa cha uchumi wa Kiislamu nchini Maritius

12:28 - May 11, 2009
Habari ID: 1776757
Kikao cha kimataifa kitakachojadili uchumi wa Kiislamu kimepangwa kufanyika katika kisiwa cha Mauritius barani Afrika tarehe 19 na 20 za mwezi huu.
Tovuti ya Afriquejet imesema kuwa kikao hicho kitajadili njia za kuimarisa uwekezaji katika Benki Kuu ya kisiwa hicho kwa kutumia mfumo wa uchumi wa Kiislamu ambao unazingatia sheria za Kiislamu. Wanauchumi, wakuu wa benki, wataalamu wa masuala ya uchumi, wanasiasa, na wahadhiri wa vyuo vikuu wa ndani na nje wapatao 200 wamealikwa kushiriki katika kikao hicho. Akizungumzia suala hilo, mkuu wa Benki Kuu ya Mauritius amesema kuwa uchumi wa Kiislamu una nafasi muhimu na nzuri sana katika mfumo wa fedha duniani na kwamba hadi sasa kungali kuna nyanja nyingi zinazoweza kutumika katika kunufaika na mfumo huo wa fedha. Mfumo wa fedha wa Kiislamu umenusurika kutokana na mgogoro wa kimataifa wa fedha na uchumi, jambo ambalo limezivutia nchi nyingi za dunia ikiwemo Mauritius, kuzingatia mfumo huo. Nchi hiyo ya Kiafrika tayari imezifanyia marekebisho sheria zake za kiuchumi na kifedha ili kunufaika na mfumo wa fedha wa Kiislamu. Mkuu wa Benki Kuu ya nchi hiyo amesema kuwa serikali iko mbioni kuruhusu kuasisiwa kwa benki za Kiislamu nchini humo. Waislamu wanachukua nafasi ya tatu kwa wingi katika jamii ya nchi hiyo baada ya Wahindu na Wakatoliki. 402595
captcha