IQNA

Msikiti wa Tokyo, sehemu ya kufanyika mazungumzo ya dini

12:28 - May 11, 2009
Habari ID: 1776761
Msikiti wa Tokyo ambao ulijengwa na Waturuki wanaoishi katika mji mkuu huo wa Japan kila siku huwapokea Wajapani wengi wa dini na mila tofauti.
Kwa mujibu wa tovuti ya DunyaBulteni ya Uturuki, Msikiti wa Tokyo ulijengwa mwaka 1935 na Waturuki waliokuwa wakiishi wakati huo katika mji mkuu huo wa Japan na kwa msaada wa moja kwa moja kutoka kwa serikali ya Uturuki, na ni kutokana na ukweli huo ndipo Wajapani wakawa wanauita kuwa ni msikiti wa Waturuki. Mbinu ya pekee ya usanifu majengo iliyotumika katika ujenzi wa msikiti huo imewavutia wengi nchini Japan jambo ambalo limewafanya wafuasi wa dini tofauti kuutembelea msikiti huo na kushiriki katika mijadala mbalimbali ya kidini ndani ya msikiti huo. Msikiti huo ulikarabatiwa mwaka 2000 na Waislamu wanaoishi katika maeneo mengine ya Japan pia walikuwa na nafasi muhimu katika ukarabati huo. 402635
captcha