Kwa mujibu wa ukurasa wa mtandao wa habari wa Zaman, wanachuo saba katika vikao hivyo vya kuhifadhi Quran Tukufu walitunukiwa vyeti katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wa serikali ya Uturuki pamoja na wageni kutoka nchi za Kenya, Ethiopia, Tanzania na Congo.
Ustadh Jamil Toker aliyeendesha darasa hizo anasema: 'Mafunzo haya ya kuhifadhi Quran Tukufu yamechukua kipindi cha mwaka moja na walio shiriki walikuwa na umari wa miaka 15-20. Wamefanikiwa katika mtihani wa kuhitimisha muhula wote wa masomo na hivyo kupokea cheti cha kuhifadhi Quran kikamilifu'.
Ameongeza kuwa, hivi sasa kuna wanachuo 33 katika chuo hicho ambao wanatazamiwa kuhitimu mwaka ujao. Ustadh Jami Toker amesema kuwa pembeni mwa mafunzo ya Quran kuna masomo mengine ya masuala ya akhlaqi. 403514