Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait la al-Watan, jumuiya ya wanachuo hao imetoa wito kupitia mtandao wake, watu na jumuiya mbalimbali za wanachuo wa Kiislamu kutoa misaada yao ya kifedha ili kununuliwa kanisa hilo na kisha kulifanya kuwa msikiti. Jumuiya hiyo ya wanafunzi imesema kuwa licha ya kuwa lengo kuu la kununuliwa kanisa hilo ni kulibadilisha kuwa msikiti kwa madhumuni ya kutekelezwa ibada lakini inaweza pia kutumika kama sehemu ya kufundishiwa masomo ya Qur'ani na masomo ya Kiislamu. Jumuiya iliyotajwa imesema kuwa tayari kuna mashirika ya masuala ya kheri na wahubiri pamoja na maimamu wa misikiti ambao tayari wamekwishatoa mchango wao kwa lengo la kununuliwa kanisa hilo. 403318