IQNA

Tamasha ya ‘Quds Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiarabu’

11:20 - May 13, 2009
Habari ID: 1777635
Tamasha ya ‘Quds Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiarabu’ katika mwaka 2009 imefanyika katika mji wa Aqaba nchini Jordan.
Kwa mujibu wa gazeti la al Dastur la nchi hiyo, hafla hiyo ilidhaminiwa na wafanya biashara wa mkoa wa Aqaba ni katika silisili ya mipango ya Jordan ya kuadhimisha kuchaguliwa Mji wa Quds kama mji mkuu wa kiutamaduni katika Ulimwengu wa Kiarabu mwaka huu wa 2009. Aidha lengo la hafla hiyo lilikuwa ni kutangaza ufungamano na taifa linalodhulumiwa la Palestina.
Mkuu wa jumuiya ya wananchi iliyoandaa hafla hiyo Ishaq Farhan amesema wameandaa hafla nyinginezo za kuuenzi mji wa Quds na kwamba harakati zao zimekuwa zikiendelea kwa mwaka moja sasa.
Katika ya yaliyojiri katika sherehe hiyo ya kiutamaduni ni tamasha za muziki, maonyesho maalumu ya kuarifisha kadhia ya Quds kwa mtazamo wa kiutamaduni na kutoa zawadi kwa watoto na familia za walioshiriki katika hafla hiyo. Baada ya kumalizika hafla hiyo baloni kadhaa zilirushwa hewani kama njia ya kutangaza ufungamano na Quds Tukufu. 404014
captcha