IQNA

Dalili za Qur'ani katika fikra ya Allama Tabatabi

14:14 - May 14, 2009
Habari ID: 1778288
Kitabu cha ad-Dilalatul Qur'aniyatu fi Fikri Muhammad Hussein Tabatabai ambacho kina kurasa 346 na kilichoandikwa na mwandishi wa Lebanon kimeonyeshwa katika kibanda cha Darul Huda Litabaa' wa Nashril wa Tauzi' ya Lebanon katika maonyesho ya kimataifa yanayooendelea mjini Tehran.
Ali Raiyya, mkuu wa mauzo na mwakilishi wa shirika hilo la uchapishaji la Lebanon katika maonyesho hayo ya 22 ya vitabu mjini Tehran amesema kuwa, shirika hilo mara hii limewasilisha vitabu mbalimbali vya utafiti wa Qur'ni katika maonyesho hayo. Mwakilishi huyo amesema kuwa shirika hilo ambalo lilishinda tuzo ya kimatifa ya duru ya 16 ya maonyesho hayo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara hii limewasilisha vitabu vipatavyo 1300. Shirika jingine la Darul Huda la nchini Lebanon ambalo linasimamiwa na Swalah Izzu Deen hadi sasa limechapisha vitabu 14 muhimu vya Kifarsi. Shirika hilo hadi sasa limekuwa na nafasi muhimu katika kueneza utamaduni na fikra ya ushia katika nchi za Kiarabu na katika ulimwengu mzima wa Kiislamu. 404494
captcha