Kwa mujibu wa gazeti la Al Wasat la Bahrain, mashindano hayo yalianza Alhamisi na yamedhaminiwa na Jumuiya ya Quran ya al Askafi ya Bahrain kwa ushirikiano na Baraza la Mji wa Manama.
Diwani katika Baraza la Mji wa Bahran Ahmad al Alawi amesema wasanii wa kazi tatu bora watatunukiwa zawadi. Ameongeza kuwa mashindano hayo yamekaribishwa na wakaazi wengi wa Bahrain.
Jumuiya ya Quran ya al Askafi imesema itaandaa mashindano kama hayo katika miji mingine ya Bahrain.
405337