IQNA

Mashindano ya Makala kuhusu Bibi Fatima Zahra (AS) Ghana

10:20 - May 17, 2009
Habari ID: 1779263
Mashindano ya kuandika makala kuhusu Bibi Fatima Zahra (AS) yameandaliwa na Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Ghana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Accra, washiriki wanaweza kuandika makala kuhusu maudhui kama vile, ‘Nafasi ya Mwanamke kwa Mtazamo wa Mtume (SAW), ‘Nafasi ya Mwanamke katika Ustawi wa Kimaanawi wa Familia’, ‘Fatima Zahra (AS) Kama Kigezo’, ‘Nafasi ya Mwanmke anayevaa Hijab katika Mwamako wa Kiislamu’, ‘Sifa za Mama wa Kiislamu’, ‘Hijabu na Heshima ya Mwanamke Katika Uislamu’, ’Nafasi ya Mwanamke katika Harakati ya Imam Khomeini (SA)’, ‘Fatima Zahra (AS) Dhihiriso la Utakasifu’, ‘Hijab na Mfungamano wa Risala’, na ‘Uimamu’. Washiriki wametakiwa kutuma makala zao katika Idara ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Accra.
Makala hizo zisizidii kurasa 20 za kawaida na zinapaswa kuandikwa kwa mojawapo ya lugha za Kiarabu, Kiingereza au Kihausa. Aidha wanaandishi wanapaswa kutaja marejeo ya makala na vile vile kiwango chao cha elimu. Makala hizo zinapokelewa kupitia anuani ifuatayo ya email: accra.icro@yahoo.com. Muhula wa mwisho wa kupokelewa makala ni tarehe 6 Juni mwaka 2006.
405840
captcha