IQNA

Makala kuhusu wanazuoni Mashia na Masunni katika mikakati ya umoja

10:21 - May 17, 2009
Habari ID: 1779266
Zaidi ya makala 80 zimetumwa katika makao makuu ya Kongamano la ‘Wanazuoni Mashia na Masunni Katika Mikakati ya Kukurubisha Madhehebu’ mkoani Golestan kaskazini mwa Iran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, makala hizo zimepokelewa na Idara ya Uenezi wa Kiislamu Mkoani Golestan.
Akizungmza na IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimin Seifullah Adabi mtaalamu wa madhehebu za Kiislamu katika Idara ya Uenezi wa Kiisalmu amesema, ‘Kongamano hili linakusudia kustawisha na kuupa nguvu utamaduni umoja baina ya madhehebu ya Kiislamu. Aidha kongamano hilo linakusudia kuleta ukuruba na maelewano ya kirafiki baina ya Maulamaa wa Madhehebu za Kiislamu ili kufikia malengo ya juu ya mafunzo ya Quran na Sira ya Mtume (SAW). Ameongeza kuwa kongamano hilo la Mwezi Julai pia litalenga kueneza mitazamo ya Imam Khomeini (SA) kuhusu umoja wa Kiislamu. 405802
captcha