IQNA

Kuakisiwa matamshi ya Kiongozi Muadhamu katika vyombo vya habari vya Kiarabu

12:56 - May 17, 2009
Habari ID: 1779310
Matamshi ya Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na njama zinazofanywa na maadui wa Uislamu kwa lengo la kuzusha fitna na hitilafu za kimadhehebu kati ya Mashia na Masuni katika mkoa wa Kurdestan nchini Iran, yameakisiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu.
Kuhusiana na suala hilo, gazeti la as-Sharqul Ausat la nchini Saudi Arabia limeandika kuwa, akizungumza huko Kurdestan, Ayatullah Khamenei amesema kuwa wale watu wanaochochea fitna na hitilafu miongoni mwa Mashia au Masuni, ima kwa kujua au kwa kutojua, ni vibaraka wa maadui wa Uislamu. Limesema kuwa Ayatullah Khamenei amesisitiza kwamba kila aina ya fitna na hitilafu miongoni mwa Mashia na Masuni ni haramu kisheria na kwamba ni jambo linalopingana wazi na mafundisho ya Qur'ani. Ama tovuti ya al-Manar ya nchini Lebanon amesema, hotuba aliyotoa Ayatullah Ali Khamenei katika Msikiti wa Ijumaa wa Sanandaj katika Mkoa wa Kurdestan, ilivunja moja kwa moja njama za maadui za kutaka kuzusha fitna na ugomvi miongoni mwa Mashia na Masuni. Tovuti hiyo imelisifu tifa la Iran kuwa ni mwamba na mlima uliosimama mbele ya njama za maadui wa kibeberu ulimwenguni na kwamba msimamo wa Kiongozi Muadhamu pamoja na taifa zima la Iran katika kuunga mkono wananchi madhlumu wa Palestina ni jambo ambalo kwa mara nyingine tena limevunja njama za maadui wa Iran za kutaka kuitenga katika ngazi za kimataifa na hasa katika eneo la Mashariki ya Kati. 405847
captcha