IQNA

Mashindano ya Makala kuhusu Quran nchini Ghana

14:08 - May 18, 2009
Habari ID: 1779617
Kumetangazwa mashindano ya uandishi makala kuhusu Quran kama mojawapo wa shughuli za pembizoni mwa mashindano ya kimataifa ya Quran Tukufu nchini Ghana.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana, makala zinapaswa kujadili maudhui kuhusu: ‘Kueneza Utamaduni wa Quran’ na ‘Kurekebisha Kigezo cha Matumizi-Kuzuia Israfu- kwa mujibu wa Quran’. Washiriki wanaweza kutuma makala zao kupitia anuani ya email ya accra.icro@yahoo.com.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Accra, makala isipungue kurasa 25 za kawaida na inaweza kuwasilisha kwa mojawapo wa lugha za Kifarsi, Kiingereza, Kiarabu, Kijerumani na Kifaransa. Makala zote zinapaswa kuwa na muhtasari pamoja na orodha ya marejeo. Aidha waandishi wanapaswa kuandika historia fupi ya maisha yao ikiwa ni pamoja na kiwango cha elimu na harakati nyinginezo za utafiti.
Muhula wa mwisho wa kupokea makala ni tarehe 10 Juni. Makala zote zitakazoidhinishwa na jopo husika zitachapishwa katika kitabu maalumu na waandishi wa makala bora zaidi watatunukiwa zawadi. 406360

captcha