Huriya Aqbani afisa anayeshusika na masuala ya Quran na Uislamu katika idara ya elimu mkoani Tehran amemuambia mwandishi wa IQNA kuwa kambi hiyo ya Qurani itajumuisha pia masuala mbali mbali ya kielimu na kiutamaduni.
Amesema katika kambi hiyo kutakuwa na vikao maalumu ya kujikurubisha zaidi na Quran Tukufu. Mbali na darasa maalumu za Quran kutakuwa pia na mafunzo kuhusu Imam Mahdi, sheria za kidini, utumizi wa kompyuta,uandishi habari n.k. 406255