IQNA

Mashindano ya Quran ya msimu wa joto Jordan

14:09 - May 18, 2009
Habari ID: 1779620
Idara ya Waqfu ya mkoa wa Rasifat nchini Jordan imetangaza kuwa itaandaa vikao vya mafundisho ya kuhifadhi na kusoma Quran Tukufu wakati wa mapumziko katika msimu ujao wa joto.
Kwa mujibu wa mwandishi wa gazeti la Al Dastur la Jordan, katika kikao cha hivi karibuni katika mkoa wa afisa mkuu wa Waqfu Rasifat kilichoongozwa na Emad al Muayata , masuala mbali mbali kuhusu mashindano hayo yalijadiliwa kwa kina. Afisa huyo wa idara ya Waqfu amesema kuna haja ya kuwepo mipango bora ya kuimarisha vituo vya kutoa mafunzo ya Quran kwani jambo hili litakuwa na mchango mkubwa katika jamii hasa kuwawezesha vijana kuhifadhi Quran Tukufu na kufahamu sheria za kidini, fiqhi na Sira ya Mtume (SAW). 406327
captcha