IQNA

Kikao cha kimataifa cha Haki za Kifedha za Mwanamke katika Uislamu

14:11 - May 18, 2009
Habari ID: 1779727
Kikao cha kimataifa cha kuchunguza haki za kifedha za mwanamke katika Uislamu kilianza siku ya Jumamosi Jeddah nchini Saudi Arabia. Kikao hicho kimeandaliwa na Kitengo cha Masuala ya Wanawake cha Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu.
Idadi kubwa ya wataalamu wa masuala ya kifedha na fiqhi ya Kiislamu kutoka nchi tofauti za Kiislamu wamealikwa kushiriki katika kikao hicho. Nabil Hatam Zare'. Mkuu wa Masuala ya Maelezo Habari na Uhusiano wa Umma wa Kituo cha Fasihi na Utamaduni cha mjini Jeddah amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, kikao cha jana Jumapili kilijadili sharia za fiqhi kuhusiana na haki za mwanamke wa Kiislamu kumiliki mali na urithi na kuzilinganisha sheria hizo na hali ya hivi sasa ya mwanamke wa Kiislamu. Amesema, makala na maoni yatakayowasilishwa katika kikao hicho yatakusanywa na kisha kuchapishwa kwa sura ya kijitabu. 406329
captcha