Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Lebanon, Mohammed Fneish ameyasema hayo akiwa mjini Sur kwa munasaba wa mwaka wa tisa wa ushindi na kukombolewa Lebanon. Ameongeza kuwa hata adui Mzayuni bado anaendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Lebanon na anajitahidi kulipiza kisasi pigo alilopata mwaka 2006 na 2000.
Naye Abdulmajid Saleh ambaye ni mjumbe katika Bunge la Lebanon amesema ametoa wito kwa makundi yote ya Lebanon kuungama ili taifa liweze kufikia malengo yake makuu. 406940