IQNA

Mashindano ya Quran katika bweni la Chuo Kikuu cha Tehran

11:07 - May 19, 2009
Habari ID: 1780319
Mashindano ya Quran kwa ajili ya wanachuo katika bweni la Chuo Kikuu cha Tehran yameanza tarehe 17 Mei na yataendelea kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, duru ya pili ya mashindano ya Quran Tukufu kwa ajili ya wanachuo wanaoishi katika bweni la Chuo Kikuu cha Tehran yanafanyika kwa viwango vya kuhifadhi Juzuu zote 30 za Quran Tukufu, Qiraa na Tartil. Mashindano ya wanaume yanafanyika katika Msikiti wa bweni la Chuo Kikuu cha Tehran huku mashindano ya wanawake yakiwa katika ukumbi wa bweni la Fatimiya.
Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Jihad ya Chuo Kikuu cha Tehran kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Harakati za Quran ya Wanachuo wa Iran, Baraza la Mji wa Tehran, Idara ya Utamaduni ya Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia na Idara ya Mabweni ya Chuo Kikuu cha Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kuna wanachuo 82 waliojisajilisha kushiriki katika kiwango cha kuhifadhi Juzuu zote 30 za Quran Tukufu, 32 katika Qiraa na 88 katika Tartil.
Leila Sangi, mkuu wa idara ya uandalizi wa mashindano hayo amesema kuwa ameelezea matumaini yake kuwa mashindano ya Quran ya wanachuo yataweza kuongeza ufungamano wao na kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu. 406856
captcha