IQNA

Wiki ya kuadhimisha Qur'ani nchini Palestina

11:01 - May 19, 2009
Habari ID: 1780337
Wiki ya kuadhimisha Qur'ani Tukufu ilianza kutekelezwa siku ya Jumapili katika miji tofauti ya Palestina. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Taasisi ya al-Furqan ya nchi hiyo.
Waandaaji wa maadhimisho hayo wanasema kuwa yana umuhimu mkubwa kwa kutilia maanani kwamba mafundisho yenye thamani kubwa ya kitabu hicho kitakatifu humletea mwanadamu saada ya humu duniani na huko Akhera pamoja na kumkinga na machafu na vilevile maovu ya kimaadili humu duniani. Akizungumzia maadhimisho hayo, Hamid Abud Abbas, Mkuu wa Chama cha Kiislamu katika eneo la an-Naqab amesema kuwa lengo la kufanyika maadhimisho hayo ni kuwashajiisha wananchi wa Palestina na hasa tabaka la vijana kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu na kudiriki maana ya mafundisho yake yenye thamani kubwa kwa mwanadamu. 406893
captcha