IQNA

Filamu ya hali halisi (documentary) ya Historia ya Kiislamu yaonyeshwa nchini Ujerumani

11:02 - May 19, 2009
Habari ID: 1780338
Televisheni ya ZDF ya nchini Ujerumani tokea jana Jumatatu imeanza kupeperusha hewani filamu ya hali halisi ya mambo inayojulikana kama al-Mashriq inayozungumzia historia ya kudhihiri Uislamu na maisha ya Mtume Muhammad (saw).
Filamu hiyo inazungumzia hatua mbalimbali za kielimu na kiutamaduni za Waislamu katika vipindi tofauti vya historian a kuathirika wananchi wa bara Ulaya na ustaarabu wa Kiislamu. Sehemu nyingine ya filamu hiyo inazungumzia hitilafu zilizojitokeza kati ya nchi za Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu na pia kuchambua matukio mbalimbali yanayojitokeza kati ya pande mbili hizo katika ulimwengu wa leo. Filamu hiyo iliyoandaliwa na Daniel Garlakh, mtaalamu wa masuala ya nchi za Mashariki, raia wa Ujerumani, imechunguzwa na kupitiwa na Sultan bin Muhammad al-Qassimi, mtawala wa Sharja, Agha Khan, mkuu wa kundi la Waismaili Duniani na idadi kadhaa ya wahadhiri na watafiti wa vyuo vikuu wa Kiislamu barani Ulaya. Filamu hiyo imetayarishwa kwa kipindi cha miaka miwili katika nchi 9 za Kiislamu. Watayarishaji wa filamu hiyo wamesema kuwa walilazimika kubadili mara kadhaa sehemu za kutengenezewa filamu hiyo kutokana na masuala ya kadhaa ya kisiasa na kijeshi, likiwemo shambulio la kinyama la hivi karibuni la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. 406927
captcha