Akibainisha suala hilo, Abu Musamah amesema kuwa matatizo yanayowakumba Waislamu wa Palestina hii leo yanatokana na kuacha kwao njia halisi na nzuri ya utamaduni na usrtaarabu wa Kiislamu na kuongeza kwamba walipaswa kutabiri matokeo mabaya ya jambo hilo. Ameendelea kusema kuwa matatizo yanayowakabili Waislamu katika nchi balimbali za Kiislamu yataondoka tu iwapo Waislamu wataamua kuzingatia historia yao ya kale na yenye fahari kubwa na kujifunza mafunzo muhimu kutokana nayo. Amesema, njia pekee ya kuwatoa katika matatizo yao ni kurejea tena katika utamaduni na ustaarabu halisi wa Kiislamu na kuamua kuwa na muamko wa kifikra katika nyanja zote za maisha yao. Amesema katika sehemu nyingine ya matamshi yake kwamba, mapambano dhidi ya dhulma inayotekelezwa dhidi ya Wapalestina na utawala haramu wa Israel yanapaswa kudumishwa. 406963