Katika mkutano wake na maafisa wa kijeshi wa Sudan akiwa safarini huko Darfur, Ehsanoglu amesema ofisi ya OIC itafunguliwa katika eneo hilo kwa lengo la kuratibu shughuli za kutoa misaada ya kibinaadamu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu amesema jumuiya hiyo ina mipango mbali mbali inayokusudia kuboresha hali ya maisha ya wakaazi wa Darfur na kwamba takribani dola milioni 485 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Ameongeza kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu inajitahidi kuhakikisha amani ya kudumu inarejea kote Sudan. 407727