Hujjatul Islam wa Muslimin Mohammad Redha Abbasi mmoja kati ya wahadhiri wa chuo cha kidini cha mjini Kermanshah nchini Iran amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa makundi yanayopotosha dini yanapata uungaji mkono wa madola yenye kiburi duniani na waitifaki wao.
Ameongeza kuwa makundi yanayopotosha ukweli kuhusu dini yalibuniwa na wakoloni. Ametoa mfano wa kundi la Uwahabbi ambalo lilibuniwa karibu karne tatu zilizopita na wakaoloni Waingereza lengo kuu likiwa ni kuibua hitillafu na uhasama baina ya Mashia na Masunni.
Hujjatul Islam wa Muslimin Mohammad Redha Abbasi ameendelea kusema kuwa makundi ya kuabudu shetani yameanziswa na Mayahudi barani Ulaya ili kuibua vita vya kiitikadi dhidi ya Waislamu na Wakristo. Amesema makundi hayo yameenea kwa kasi katika maeneo mbali mbali duniani.
Mhadhiri huyo wa masuala ya kidini ametoa wito kwa vyombo vya habari vya Kiislamu kuanzisha mikakati maalumu ya kufichua makundi hayo potofu na kutoa miongozo sahihi ya kidini. 407836