IQNA

Khitma ya Quran ya Ayatollah Bahjat kupitia intaneti

13:42 - May 20, 2009
Habari ID: 1780677
Tovuti ya habari ya Tebyan imeandaa khitma ya Quran Tukufu kupitia intaneti kufuatia kuaga dunia Ayatullahil Udhma Bahjat.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti hii inayofungamana na Shirika la Uenezi wa Kiislamu imechapisha makala mbali mbali kuhusu maisha ya marhum Ayatullah Bahjat na vile vile kuandaa khitma ya Quran.
Wanablogu katika tovuti hiyo wanafursa kunazia tarehe 19 -29 Mei kushiriki katika khitma hiyo ya Quran.
Ayatullah Mohammad-Taqi Bahjat, Marja’a wa ngazi za juu wa Kishia aliaga dunia tarehe 17 Mei katika mji mtakatifu wa Qom nchini Iran akiwa na umri wa miaka 96. Ni mwanazoni aliyebobea katika masomo ya kidini na alikuwa na mamillioni ya wafuasi kote duniani.
Waumini wanaotaka kushiriki katika khitma hii ya Quran wanaweza kufanya hivyo kupitia ukurasa wa intaneti wenye anuani ifuatayo
http://www.tebyan.net/index.aspx?pid=46525
407627
captcha