Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, khitma hiyo ya Quran imeandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zambia. Kati ya wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Mufti wa Zambia Sheikh Asadullah Mwale, viongozi wa Jumuiya kadhaa za Kiislamu za Masunni na vile vile Mashia waishio nchini humo kutoka Lebanon, India, Pakistan.
Khitma nyingine ya Marhum Ayatullahil Udhma Bahjat itafanyika tarehe 22 Mei katika Masjid Nabi (SAW) eneo la Kutuba na pia katika Msikiti wa Imam Redha (AS) mjini Livingstone. 407888