IQNA

Vipofu wa China wajifunza kusoma Qur'ani

15:51 - May 20, 2009
Habari ID: 1781003
Sulban Khasimikof, katibu wa vyombo vya habari wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu wa China ametangaza habari ya kuanza masomo ya usomaji Qur'ani kwa vipofu wa nchi hiyo, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa jambo hilo kutekelezwa nchini humo.
Akifafanua suala hilo, Katibu Khasimikof amesema kwamba mwaka uliopita Darul Fatuwa ya China ilituma watu 12 katika Kituo Maalumu cha Usomaji Qur'ani kwa Vipofu huko Kazan, mji mkuu wa Tataristan kwa lengo la kupata masomo ya jinsi ya kuwafunza vipofu kusoma Qur'ani na kwamba baada ya kuhitimu masomo yao sasa wana uwezo wa kutoa masomo hayo kwa vipofu wa China. Amesema walipata masomo hayo katika kipindi kifupi na kwamba wanashirikiana na Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu wa China kwa lengo la kutoa huduma zao kwa vipofu wa nchi hiyo. Amesema kuwa kituo kilichotajwa cha kutoa masomo ya usomaji Qur'ani kwa vipofu ya Tatarestan nchini Russia ndicho kituo cha pekee nchini humo kinachotoa masoamo hayo maalumu. Kwa mujibu wa takwimu za Jumuiya ya Vipofu ya Russia, kuna vipofu wapatao 2500 nchini China ambapo 1500 kati yao hawana macho yote mawili. 407604
captcha