Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Imarati, WAM, maonyesho hayo yanaendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha mjini Dubai. Zaidi ya mabango 70 ya picha za wanagrafia na wachoraji mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu ambayo yanaonyesha aya za Qur'ani yamewekwa kwa ajili ya kutazamwa na wapenzi wa sanaa hiyo ambayo itaendelea kuonyeshwa kwa muda wa wiki moja. Vilevile vikao mbalimbali vitafanyika pembeni ya maonyesho hayo ambapo hotuba mbalimbali zinazohusiana na sanaa ya kaligrafia ya aya za Qur'ani zitatolewa. Waandaji wa maonyesho hayo wanasema kuwa lengo kuu la kufanyika kwake ni kuimaisha sanaa ya kaligrafia ya uandishi wa aya za Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwaonyesha wapenzi wa sanaa hiyo athari zake. Maonyesho hayo yameandaliwa na Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Dubai kwa ushirikiano wa Benki ya Kiataifa ya Dubai, Tasisi ya Televisheni na Radio ya Dubai pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Fedha cha mjini humo. 408349