Akizungumzia suala hilo, Talib Abu Shi'r, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Palestina amesema kuwa watafiti wa ulimwengu wa Kiislamu na wanafikra wa nchi mbalimbali wanaweza kushiriki katika mashindano hayo kwa kuwasilisha kazi zao za utafiti na kielimu kuhusiana na 'fadhila na karama za kimaadili za Mtume Muhammad (saw) na Uislamu, dini ya amani na usawa.' Amesema wizara yake itakuwa na jukumu la kukusanya na kuchagua kazi bora zaidi na kutoa zawadi nono kwa washindi wa mashaindano hayo. Waziri huyo pia ametoa habari ya kuanzishwa duru za uchunguzi na utafiti wa nuskha za maandishi ya mkono ya Kiislamu na kusisitiza kwamba hati hizo za mkono ni jambo linalozingatiwa na kupewa umuhimu mkubwa katika nchi za Magharibi. Amesema, hii ni katika hali ambayo hati hizo za mkono hazipewi umuhimu mkubwa katika nchi za Kiislamu na Kiarabu. 408260