Kikao cha nane cha kimataifa cha jumuiya za kidini zinazosimamia Mashirika ya kifedha ya Kiislamu kilianza siku ya Jumanne katika mji wa Manama, Bahrain. Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la nchi hiyo GNA, wawakilishi wa jumuiya za kidini zinazosimamia shughuli za kiuchumi na miamala ya kibiashara ya mashirika ya kifedha na benki za Kiislamu wanashiriki katika kikao hicho.