IQNA

Kikao cha Wafuasi wa Tamaduni na Dini Tofauti nchini Saudi Arabia

11:53 - May 21, 2009
Habari ID: 1781157
Kikao cha kimataifa cha 'kuchunguza mauamala wa mwanadamu na mawasiliano na wafausi wa dini na tamaduni mbalimbali katika mtazamo wa Qur'ani Tukufu kilianza siku ya Jumanne huko mjini Qatif Saudi Aarabia, ambapo idadi kubwa ya maulamaa na watafiti wa masuala ya Qur'ani wamehudhuria.
Akizungumza katika kikao hicho, Sheikh Faisal al-Awami, Mkuu wa Taasisi ya Qur'ani ya Nur ya mjini Qatif amesema kuwa katika kitabu hicho kitakatifu Mwenyezi Mungu anamtaka mwanadamu kuamiliana na wenzake kwa msingi wa amani na kwamba Hawataki kutumia njia za mabavu na nguvu katika miamala yao. Amesema, kuna baadhi ya maadui wa Uislamu ambao wanatumia vibaya aya ambazo Mwenyezi Mungu anawahusia Waislamu kufanya jihadi katika baadhi ya sehemu na kudai kwamba Qur'ani ni kitabu kinachowashajiisha wafuasi wake kutumia nguvu na kujaribu kuonyesha kwamba kinawachochea wafuasi wake kuwaua wenzao. Hii ni katika hali ambayo Qur'ani na aya zinazohusiana na jihadi na kupigana kwa njia ya Mwenyezi Mungu zinatekelezwa tu katika hali ya kujitetea na kujilinda na katika hali ya dharura tu. Amesisitiza kwamba, muamala wa mwanadamu na wenzake kwa mtazamo wa Qur'ani umesimama juu ya msingi wa amani na kwamba wataalamu wa fiqhi ya Kiislamu wamebuni sheria madhubuti zinazohusiana na jihadi na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kwamba, jihadi inapasa kufanywa kwa ajili ya kukabiliana na makafiri, watawala dhalimu na watu walioritadi. 408186
captcha