IQNA

Obama kutunukiwa nakala ya Qur'ani Tukufu

15:29 - July 04, 2009
Habari ID: 1798353
Baraza la Uhusiano wa Kiislamu Na Marekani CAIR limepanga kumtunuku Rais Barack obama wa Marekani nakala ya Qur'ani iliyofasiriwa kwa lugha ya Kiingereza.
Sherehe za kumkabidhi Obama nakala hiyo ya tarjumi ya Qur'ani itafanyika tarehe 15 mwezi huu wa Julai ikiwa ni katika kutekeleza mpango kugawa nakala laki moja za tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa viongozi mbalimbali wa serikali ya Marekani.
Mkurugenzi wa Masuala ya Mawasiliamo wa jumuiya ya CAIR Feith Ali amesema kuwa mpango huo unatekelezwa ili kuwashawishi viongozi wa Marekani waruhusu mafunzo ya Kiislamu katika shule za nchi hiyo.
Amesema kuwa malengo mengine ya mpango huo ni kuwaelimisha viongozi na wananchi wa Marekani thamani za Qur'ani Tukufu na kusahihisha mtazamo wao kuhusu Uislamu.
Mpango wa kugawa nakala laki moja za tarjumi ya Qur'ani kwa viongozi wa serikali, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu na maafisa wa ngazi za juu wa polisi ya Marekani wabunge na wanahabari ulianza kutekelezwa tarehe 30 Juni mwaka huu.
428958

captcha