IQNA

Mkutano wa Mustakbali wa Uislamu waanza Marekani

18:35 - July 11, 2009
Habari ID: 1800517
Mkutano wa Mustakbali wa Uislamu nchini Marekani ulianza kazi zake jana katika mji wa Jackson kwenye jimbo la Mississippi.
Mkutano huo utakaoendelea kwa siku tatu unahudhuriwa na zaidi ya viongozi na Waislamu 500 kutoka maeneo yote ya Marekani.
Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ya Waislamu wa Marekani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani CAIR Nihad Awadh amehutubia kikao cha ufunguzi wa mkutano huo akiashiria ongezeko la wimbi la chuki na uhasama dhidi ya Uislamu na akasema, njia pekee ya kukabiliana na hujuma hiyo ni kueneza maarifa na elimu kati ya wafuasi wa dini mbalimbali. Amesema kuwa kuna udharura wa kuwaelimisha watu kuhusu Uislamu na kuwafahamisha kwamba ni dini ya amani, uadilifu na upendo.
Mkutano huo utakalimisha shughuli zake kesho Jumapili. 431688
captcha