IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kuanza kesho mjini Tehran

19:10 - July 18, 2009
Habari ID: 1803522
Mashindano ya 26 ya kimataifa ya Qur'ani yatanaaza kesho mjini Tehran yakiwashirikisha washindani kutoka nchi 52. Mashindano hayo yataanza sambamba na maadhimisho ya siku ya kubaadhiwa Mtume Muhammad (saw).
Mashindano hayo yatafunguliwa na Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran Ayatullah Mahmoud Hashimi Shahroudi.
Zaidi ya washindani 80 kutoka nchi 52 duniani wamekwishawasili nchini Iran kwa ajili ya mashindano hayo.
Majaji wa mashindano hayo ya kimataoifa ya Qur'ani wanatoka nchi za Syria, Iraq, Uturuki, Yemen, Misri na mwenyezi Iran.
Sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zitafanyika Ijumaa ijayo kwa hotuba ya Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 435389
captcha