Kongamano hilo litahudhuriwa na wasomi, wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali duniani katika Chuo Kikuu cha Kerala. Mkuu wa Kitengo cha Lugha ya Kiarabu cha Chuo Kikuu cha Kerala A. Nizarudeen amesema mada kuu ya kongamano hilo ni nafasi ya lugha ya Qur'ani Tukufu katika elimu na sayansi.
Masuala mengine yatakayochunguzwa katika kongamano hilo la kimataifa ni muundo wa Qur'ani Tukufu, tafsiri za Qur'ani katika vipindi mbalimbali, njama za kupotosha maandiko ya Qur'ani, kaligrafia ya Qur'ani, Qur'ani za digitali na kadhalika.
Kongamano hilo pia litafanyika sambamba na vikao vya kiraa ya Qur'ani, mashindano na maonyesho ya kitabu hicho kitukufu cha Mwenyezi Mungu. 555063