IQNA

Uchunguzi wa maoni wa Gallup umebaini:

Asilimia 63 ya Wamarekani hawajui chochote kuhusu Uislamu

10:42 - March 31, 2010
Habari ID: 1901033
Ripoti ya hivi karibuni kabisa ya taasisi ya uchunguzi wa maoani ya Gallup ya Marekani imesema kuwa asilimia 63 ya raia wa Marekani hawajui chochote kuhusu dini ya Kiislamu.
Ripoti ya Gallup ambayo inabeba kichwa cha habari: "Mitazamo ya kidini nchini Marekani na uchambuzi wa kina kuhusu mielekeo ya Wamarekani juu ya Uislamu na Waislamu" imesema asilimia 63 ya raia wa Marekani wamesema katika uchunguzi wa maoni kwamba hawajui lolote kuhusu dini ya Kiislamu na kwamba wana ufahamu finyu mno kuhusu dini hiyo.
Ripoti ya Gallup inasema vyombo vya propaganda vya Marekani vinamuarifisha mwanamke Muislamu kuwa ni mhanga, suala ambalo linawafanya raia wa nchi hiyo wahukumu kwamba hakuna usawa baina ya mwanamke na mwanaume katika dini ya Kiislamu. Ripoti hiyo imesisitiza kuwa suala hilo lina taathira kubwa katika kuimarisha mtazamo usiokuwa sahihi wa Wamarekani kuhusu Uislamu.
Wakati huo huo Mahmoud Ashur, wakili wa zamani wa Chuo cha al Azhar cha Misri amesema ujahili na ujinga wa Wamarekani na Wamagharibi kwa ujumla kuhusu dini ya Kiislamu imechangiwa kwa kiasi fulani na udhaifu wa mipango ya vyombo vya habari vya Waislamu na uwezembe wa wafuasi wa dini hiyo katika kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa raia wa Marekani na jamii za nchi za Magharibi. 555844


captcha