Gazeti la al Fajr el Jaded limeandika kuwa mashindano hayo yanasimamiwa na Idara ya Waqfu ya jiji la Tripoli ikishirikiana na vituo 50 vya mafunzo ya Qur'ani.
Mashindano hayo yanajumuisha sekta za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 na juzuu saba za mwisho za kitabu hicho.
Mkuu wa Idara ya Waqfu ya Tripoli amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya Qur'ani ni kuhamasisha vijana kuhifadhi Qur'ani na kuwatayarisha kwa ajili ya mashidano ya kimataifa ya kitabu hicho kitakatifu. 560475