IQNA

Mashindano ya 27 ya Kimataifa ya Quran yamalizika Tehran

12:08 - July 16, 2010
Habari ID: 1956408
Mashindano wa 27 ya kimataifa ya Quran Tukufu yamemalizika Jumatano usiku mjini Tehran. Mashindano hayo yalikuwa katika viwango vya Kuihifadhi Quran Tukufu na Kuisoma Quran Tukufu kwa mujibu wa Tajweed.
Mashindano hayo yalikuwa katika viwango vya Kuihifadhi Quran Tukufu na Kuisoma Quran Tukufu kwa mujibu wa Tajweed. Washindi walikuwa kama ifuatavyo; katika kitengo cha Qiraa au kuisoma Quran tukufu nafasi ya kwanza imechukuliwa na Masoud Nikdasti kutoka Iran, nafasi ya pili imechukuliwa na Abdullah Dawud Mohammad kutoka Tanzania na nafasi ya tatu imechukuliwa na Fathullah Wahiyudin kutoka Indonesia. Na katika kitengo cha kuhifadhi kikamilifu Quran tukufu nafasi ya kwanza imechukuliwa na Ali Rajabi kutoka Iran nafasi ya pili imechukuliwa Mahdi Mohammad Khalil kutoka Iran huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Abdul Al Hafidh al Hadi kutoka Libya. Mashindano hayo yamemalizaka kwa hotuba ya Ayatollah Amoli Larijani Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran. Mashindano hayo yamemalizaka kwa hotuba ya Ayatollah Amoli Larijani Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran. Washiriki 95 kutoka nchi 60 duniani walishiriki katika mashindano hayo. Mashindano hayo hufanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya Tarehe 27 ya mwezi wa Rajab, siku aliyobaathiwa na kupewa Utume Mtume Muhammad SAW.
captcha