IQNA

Mtoto wa Miaka minane ashinda mashindano ya Quran Makka

10:24 - July 27, 2010
Habari ID: 1962632
Mvulana mwenye umri wa miaka minane amechukua nafasi ya kwanza katika mashindano maalumu ya watoto ya kuhifadhi Quran Tukufu yaliyofanyika katika mji mtakatifu wa Makka.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Madina, mashindano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Quran Tukufu mjini Makka na kuhudhuriwa na watoto 2000.
Kwa mujibu wa msimamizi wa jumuiya hiyo Nawaf Al Ghalib, mshindi alijibu kwa njia sahihi maswali yote kuhusu kuhifadhi Quran Tukufu mbali na kusoma kwa kuzingatia hukumu zote za Tajweed na hivyo akafanikiwa kupata alama 100. Bw. Ghalib amesema jumuiya yake inajitahidi kutoa mafunzo bora ya kuhifadhi Quran Tukufu na ndio sababu mshindi ni mwanafunzi wa jumuiya hiyo ambayo pia hujihusisha na masuala ya kutoa misaada.
Ameongeza kuwa jumuiya hiyo sasa ina wanafunzi 800 ambao wamehifadhi kikamilifu Quran Tukufu huku wanafunzi wengine 1500 wakiwa wamefanikiwa kuhifadhi Juzuu 15 za Quran Tukufu.
620883

captcha