IQNA

Mwanazuoni wa Al Azhar ataka itikadi ya Umahdi ienezwe

10:24 - July 27, 2010
Habari ID: 1962633
Mwanazuoni mmoja wa Chuo Kikuu cha Al Azhar amesema kunapaswa kutumiwa mkakati maalumu wa kiutamaduni kuarifisha itikadi ya Umahdi na kuwapa bishara njema wanaadamu kwani wote waliodhulumiwa na wapendao uhuru wanasubiri aliyeahidiwa ambaye ni Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake).
Kwa mujibu wa ripota wa Shirikal la Habari la Qurani IKNA aliyehudhuria Kogamano la Sita la Kimataifa Kuhusu Itikadi ya Umahdi mjini Tehran, Sheikh Ahmad Abdul Rahim As Saiih ambaye ni Mhadhiri wa falsafa na itikadi katika Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri amesema: "Ubeberu wa magharibi ungali unataka kueneza satua katika nchi za Kiislamu hasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivi sasa mabeberu hao wanalenga kuhujumu itikadi ya Umahdi kwa mbinu mbali mbali". Mwanazuoni huyo wa Al Azhar ameashiria njia za kupambana na wale wanaopinga itikadi kumhusu Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) na kusema: "Tunapaswa kuimarisha fikra, utamaduni na harakati mbali mbali za kielimu katika nyanja hii ili kuvunja njama za wanaopinga Umahdi".
Inafaa kukumbusha hapa kuwa miaka 1176 iliyopita yaani tarehe 15 Shaaban 255 Hijria alizaliwa Imam Muhammad al Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) mmoja kati ya watu wa nyumba tukufu ya Mtume Muhammad SAW katika mji wa Samarra nchini Iraq. Kabla ya kuzaliwa kwake, madui wa dini tukufu ya Kiislamu walijaribu kuzuia kuzaliwa kwa shakhsia huyo kwani walifahamu kwamba angelidhihiri na kuleta uadilifu na usawa kwa wanadamu wote duniani. Mtume Mtukufu SAW alisikika akisema kuwa, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) anatokana na kizazi chake na alikuwa akiwabashiria Waislamu juu ya kudhihiri kwake katika zama za mwisho ambapo ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa baada ya kuwa umejaa dhulma, uonevu, fitina, hitilafu na ukosefu wa usalama.
620703

captcha