IQNA

Jihad Islami:

Mapambano ndio njia pekee ya kumshinda adui Mzayuni

21:24 - August 06, 2010
Habari ID: 1967924
Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kwamba mapambano ndio njia pekee ya kumshinda adui na kukomesha uchokozi na dhulma zake. Jihad Islami imesema njia ya mapambano inaimarika zaidi siku baada ya siku.
Taarifa iliyotolewa na Jihad Islami kwa mnasaba wa kukumbuka ushindi wa harakati ya Hizbullah katika vita vya siku 33 dhidi ya Wazayuni maghasibu imelipongeza jeshi la Lebanon na mapambano ya Kiislamu yaliyoongozwa na Hizbullah.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Lebanon na harakati zote za mapambano zinaadhimisha ushindi uliopatikana katika vita vya siku 33 ambapo Hizbullah ilidhihirika kama nembo ya mapambano na ushindi.
Taarifa ya Jihad Islami pia imeashiria shambulizi lililofanywa juzi na jeshi la utawala ghasibu wa Israel huko kusini mwa Lebanon na kusisitiza kuwa kwa mara nyingine tena jeshi la kigaidi la Israel limeshambulia eneo la kusini mwa Lebanon na kwamba mapambano ya jeshi la Lebanon dhidi ya mashambulizi hayo na mapigano yaliyotokea yamepelekea kuuawa shahidi wananchi kadhaa na kuangamizwa afisa wa ngazi za juu wa Israel.
Jihad Islami imepongeza mapambano ya jeshi la Lebanon katika tukio hilo. 626564
captcha