Siku ya Ijumaa OIC ilizitaka taasisi na mashirika yake yote kushirikiana kwa karibu na kuwasilisha mipango na sera zao kuhusiana na Afghanistan. Mashirika muhimu ya jumuiya hiyo ikiwemo Benki ya Ustawi ya Kiislamu IDB na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Kiislamu ISESCO yameombwa kufanikisha kikao hicho kijacho kwa kushirikiana kwa karibu kuhusu suala hilo. Jumuiya hiyo pia imetangaza kuwa wawakilishi wa taasisi na mashirika hayo watafanya safari nchini Afghanistan na kubadilishana mawazo na viongozi wa nchi hiyo kabla ya kufanyika kikao kilichotajwa. Wawakilishi hao pia watachunguza mipango na miradi inayotekelezwa na OIC nchini Afghanistan. Pendekezo la kufanyika kikao hicho cha mawaziri lilitolewa katika kikao cha kimataifa huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan na Ahmad Abul Ghait, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, tarehe 21 mwezi Julai. Washiriki wa kikao hicho pia waliitaka OIC kuimarisha zaidi juhudi zake katika utatuzi wa mzozo wa Palestina.
627995