IQNA

Shirika la kwanza la huduma za ndege kwa ajili ya mahujaji nchini Morocco

10:27 - August 09, 2010
Habari ID: 1969617
Kutokana na juhudi za Shirika la Ndege la al-Wafir la nchini Saudi Arabia, shirika la kwanza la huduma za ndege kwa ajili ya mahujaji lilifunguliwa siku ya Jumamosi tarehe 7 Agosti huko katika mji wa Aghadir nchini Morocco.
Akizungumzia suala hilo, Muhammad Husna mkuu wa shirika hilo la al-Wafir amesema kuwa ndege ya kwanza ya shirika hilo iliondoka katika mji huo kuelekea Jeddah Saudia ikiwa na abiria 450 na kwamba tokea sasa mahujaji wote wa hija ya umra na tamatu' watakuwa wakifanya safari zao nchini Saudia kupitia shirika hilo. Amesema shirika hilo limefurahishwa sana na fursa iliyotolewa na viongozi wa Morocco ya kuendesha shughuli zao nchini humo. Mbali na Morocco shirika hilo pia lina shughuli za kupeleka mjini Makka mahujaji wa nchi nyinginezo za Kiislamu.
Muhammad Husna ameelezea matumaini yake kwamba shirika hilo litatekeleza vyema jukumu lake la kuwasafirisha mahujaji wa Morocco kuelekea Saudi Arabia bila kukabiliwa na matatizo makubwa. 628666
captcha