Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika ICRO Mohsen Pakayeen amesema maqari 50 wa kimataifa pamoja na makundi 20 ya Qaswida yatatumwa katika nchi mbali mbali katika Mwezi wa Ramadhani. Ameongeza kuwa ICRO inasimamia kitengo cha wachapishaji wa kimataifa katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu yaliyoanza Jumamosi usiku mjini Tehran. Maonyesho hayo ambayo yana washiriki kutoka nchi 25 duniani yatamalizika tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
628083