Maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika mwezi mzima wa Ramadhani hadi siku ya Idul Fitr yataonyesha Qur'ani iliyochapishwa katika nakala mbalimbali, CD zilizo na maudhui mbalimbali za kidini na vitabu vya Kiislamu vilivyochapishwa katika lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.
Vilevile programu za vitabu vinavyoonyeshwa katika maonyesho hayo zitauzwa kwa upungufu wa bei wa asilimia 20. Walio na hamu ya kuyatembelea maonyesho hayo wanaweza kufanya hivyo tokea asubuhi hadi wakati wa kufuturu. Wanaweza pia kuyatembelea maonyesho tokea saa mbili hadi saa sita usiku. 630453