Kikao hicho kimeandaliwa na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Misri. Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar, Muhmoud Hamdi Zaqzouq, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu na Ali Jumua' Mufti wa Misri ni miongoni mwa shakhsia mashuhuri wa nchi hiyo watakaohudhuria kikao cha ufunguzi cha mkutano huo wa Kiislamu.
Mufid as-Shahab, Waziri wa Masuala ya Sheria na Bunge, Mushirat Khitab, Waziri wa Nyumba na Familia na Ali Deen Hilal, Katibu Mkuu wa Vyombo vya Habari wa Chama cha Taifa cha Misri ni shakhsia wengine mashuhuri watakaohutubu katika kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuchunguza maudhui mbalimbali zinazohusiana na fikra ya Kiislamu.
Vilevile Ahmad Omar Hashim, mkuu wa Kamisheni ya Masuala ya Kidini ya Bunge la Misri, Khalid al-Jundi mmoja wa wanazuoni wa Misri na Mahmoud Ashur, wakili wa zamani wa al-Azhar ni miongoni mwa shakhsia wengine wa Misri watakaohudhuria na kutoa hotuba katika kikao hicho. 630677