IQNA

Mashindano ya Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani Imarati

11:09 - August 11, 2010
Habari ID: 1971247
Awamu ya mwisho ya duru ya tano ya mashindano ya Qur'ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yatafanyika katika mji wa Sharja Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mashindano hayo yanafanyika chini ya usimamizi wa clabu ya masuala ya kiutamaduni na michezo ya Ladhidh katika mji wa Sharja ikishirikiana na Taasisi ya Qur'ani na Suna za Mtume (saw) ya mji huo.
Msimamizi wa mashindano hayo Qasim Muhammad Fadhil amesema kuwa awamu ya kwanza ya mashindano hayo ilifanyika tarehe 8 na 9 mwezi huu wa Agosti ikishirikisha washindani 150 katika nyanja za kuhifadhi juzuu 20, 15, 10, 5 na 2 za Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa watu 40 waliofanikiwa kupata alama 90 katika awamu ya kwanza ya mashindano hayo wamechaguliwa kushiriki katika awamu yake ya mwisho iliyopangwa kufanyika tarehe 10 za mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 630666
captcha