IQNA

Baadhi ya nchi za Kiislamu zaanza saumu Jumatano

13:53 - August 11, 2010
Habari ID: 1971519
Nchi kadhaa za Kiislamu leo zimeanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Taasisi husika katika nchi kama Indonesia, Malaysia, Saudi Arabia, Misri, Imarati, Libya, Qatar, Kuwait, Lebanon, Uturuki, Yemen ,Palestina, Tunisia na Algeria zimetangaza Jumatano ya leo tarehe 11 Agosti kuwa tarehe mosi mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwezi mtukufu wa Ramadhani katika maeneo mengine unatarajiwa kuanza kesho Alkhamisi. Hapa nchini Iran makundi mbalimbali ya kusaka mwezi mwandamo hayakuweza kuona mwezi Jumanne jioni na kwa msingi huo leo imetangazwa kuwa ni siku ya mwisho ya mwezi wa Shaaban.
Huko Afrika mashariki na kati pia Waislamu katika nchi za Rwanda na Uganda wameanza leo kutekeleza ibada ya funga ya Ramadhani. Nchini Kenya aghalabu ya Waislamu wanatazamiwa kuanza kufunga hapo kesho Alhamisi kufuatia tangazo la Kadhi Mkuu wa Nchi hiyo.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu SW aujalie mwezi wa rehma, baraka na maghufira kwa Waislamu wote na atakabali dua na sala zetu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
631055


captcha